2 Kings 21:18-20

18 aManase akalala pamoja na baba zake na akazikwa katika bustani ya jumba lake la kifalme, katika bustani ya Uza. Naye Amoni mwanawe akawa mfalme baada yake.

Amoni Mfalme Wa Yuda

(2 Nyakati 33:21-25)

19Amoni alikuwa na miaka ishirini na miwili alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka miwili. Mamaye aliitwa Meshulemethi binti Haruzi, kutoka Yotba. 20 bAkatenda maovu machoni mwa Bwana, kama baba yake Manase alivyofanya.
Copyright information for SwhNEN